Sunday 14 June 2015

TUNZA MAZINGIRA KWA MAISHA YA KESHO

Mazingira ni vitu vyote vinavyotuzunguka vyenye uhai na visivyo na uhai. Vitu vyenye uhai ni pamoja na mimea na wanyama na visivyo ni pamoja na uhai ni hewa, ardhi na maji. Mazingira yanahusisha pia vitu vyote vinavyosaidia kuendelea kuwepo kwa maisha ya mwanadamu na viumbe wengine. Hivyo basi maisha ya viumbe hai wa kizazi kilichopo na kijacho kinategemea uwepo wa mausiano mazuri kati ya watu namazingira.
 
Juhudi za Serikali katika kutunza Mazingira
Kuzuia uchimbaji haramu wa kokoto, mchanga na vifusi
Katika kudhibiti uharibifu wa ardhi kutokana na uchimbaji holela wa kokoto, vifusi na mchaga, Uongozi  ulitoa tamko linalozuia shughuli hizo katika Mamlaka za Serikali za Mitaa katika Mikoa mbalimbali Tanzania.
Kutoa elimu ya usafi na utunzaji wa mazingira
Mamlaka za Serikali za Mitaa katika Mikoa mbalimbali Tanzania zinawajibika kusimamia usafi wa mazingira. Wajibu huo unafanyika kwa kushirikisha ngazi zote za serikali na wadau mbalimbali kama vile sekta binafsi na wakazi katika ngazi ya kaya.

Usimamizi wa sheria za utunzaji wa mazingira
Mamlaka za Serikali za Mtaa katika Mikoa mbalimbali Tanzania zina sheria zinazohusu utunzaji, uhifadhi na uendelevu wa mazingira. Katika kusimamia sheria hizo, shughuli zinazofanyika katika maeneo yasiyoruhusiwa huondolewa. Nakuhakikisha kila Halmashauri kushiriki kwa kufanya shughuli mbalimbali za usafi na uhifadhi mazingira katika maeneo mbalimbali.
 
 
 

 
 
 
 
 
 
 

 


 
 MAZINGIRA BORA KWA MAISHA



     Usafi wa mazingira

Usafi wa mazingira ni njia ya kuendeleza afya kwa kuzuia mawasiliano ya binadamu na athari za taka. Athari hizo zinaweza kuhusu mwili, mikrobiolojia, biolojia au kemikali vikolezo vya ugonjwa.
Taka ambazo zinaweza kusababisha matatizo ya afya ni kinyesi cha binadamu na wanyama, taka ngumu, maji machafu, taka za viwandani, na taka za kilimo.
Usafi kama njia ya kuzuia maradhi unaweza kutumika kwa ufumbuzi handisi (kama majitaka na tiba ya maji machafu), teknolojia rahisi kama vyoo, au matendo ya usafi binafsi (kama uoshaji wa mikono kwa sabuni).
Usafi wa mazingira kama unavyoelezwa kwa ujumla na Shirika la Afya Duniani (kwa Kiingereza World Health Organisation, kifupi WHO), unahusu utoaji wa vifaa na huduma ya usalama wa mkojo na kinyesi cha binadamu.
Upungufu wa usafi wa mazingira ni sababu kuu ya maradhi duniani kote. Uboreshaji wa mazingira una manufaa makubwa kwa afya ya wote katika kaya na katika jamii.

Usafi wa mazingira unahusu pia udumishaji wa ratiba ya usafi, kwa njia ya huduma kama vile ukusanyaji wa taka na maji machafu.